Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani ameyashuruku majeshi ya Marekani yaliyopelekwa nchini mwake miaka 14 iliyopita. Shukrani hizo amezitoa jana wakati wa ziara yake rasmi ya kwanza nchini Marekani, tangu alipoingia madarakani mwaka uliopita. Ghani aliyeambatana na Mtendaji Mkuu wa Afghanistan, Abdullah Abdullah, amezishukuru juhudi zilizofanywa na wanajeshi wa Marekani nchini kwake. Aidha, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Ashton Carter, ameihakikishia Afghanistan kuwa nchi yake itaendelea kuvisaidia kifedha vikosi vya usalama vya Afghanistan. Rais Ghani ambaye pia amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, leo anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais Barack Obama, katika Ikulu ya Marekani
24 Machi 2015 - 09:12
Msimbo wa Habari: 678680
Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani ameyashuruku majeshi ya Marekani yaliyopelekwa nchini mwake miaka 14 iliyopita